Mh. Amon Chakushemeire, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mzumbe (MUSO) amefanya uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali na kuwahamisha Wizara baadhi ya Manaibu Waziri. Katika uteuzi huo baadhi ya Manaibu Waziri wamepandishwa hadhi na kuwa Mawaziri kamili wa Wizara. Manaibu Waziri waliopandishwa hadhi ya kuwa Mawaziri ni pamoja na Mh. Judith Kweka aliyekuwa N/Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge na kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mh. Hamis Mbawala aliyekuwa N/Waziri wa Wizara ya Mikopo, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Wizara ya Mikopo, Mh. Vaileth Lusana Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Teknolojia na Mafunzo ya Sanaa, amekuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo, Mh. Mfaume Mfaume aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya, Chakula na Mahusiano amekuwa Waziri katika Wizara hiyo, Mh. Albert Nzilolela Naibu Waziri Wizara ya Habari na Mawasiliano kwa sasa ni Waziri wa Wizara ya Habari na Mawasiliano na Mh. Lydia Yohana aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Mazingira, Maji na Nishati amekuwa Waziri wa Wizara husika.
Aidha Mh. Rais amefanya mabadiliko katika Wizara mbalimbali kwa kufanya uteuzi wa Mawaziri, Manaibu Waziri na Katibu wa Kudumu wa Wizara, Mawaziri waliobahatika kuteuliwa katika nafasi hizo ni Mh. Grace Kasebele Waziri wa Wizara ya Sheria na Katiba, Mh. John Lameck Waziri Wizara ya Malazi na Miundombinu, Joseph Kapyunka Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Teknolojia na Mafunzo ya Sanaa, Mh. Robert Tende Naibu Waziri wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo na Mh. Gigwa Mipawa Katibu wa Kudumu Wizara ya Elimu, Teknolojia na Mafunzo ya Sanaa.
Ili kuleta ufanisi na tija katika utendaji kazi, Mh. Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mzumbe (MUSO) amefanya mabadiliko mbalimbali kwa kuwahamisha Wizara baadhi ya Manaibu Waziri wa wizara mbalimbali. Manaibu waliohamishwa Wizara ni pamoja na Mh. Ebenezer F. Elishiwanga kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na kuhamishiwa Wizara ya Sera, Uratibu na Shughuli za Bunge na Mh. Hellen Said aliyekuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Fedha, Mipango na Uwekezaji amekuwa Naibu Waziri Wizara ya Sera, Uratibu na Shughuli za Bunge.
Zaidi, Mh. Rais wa Serikali ya Wanafunzi Mzumbe (MUSO) amewaapisha Wateule hao na kuanza kazi mara moja katika nafasi walizoteuliwa mara baada ya kula kiapo hicho. Mara baada ya kuwaapisha, Mh. Rais amewakumbusha kuwa na moyo wa kuwatumikia Wanachuo na kuwaasa kutii kiapo hicho kwa kuzingatia maneno yaliyomo na maadili ya Uongozi.
No comments:
Post a Comment