Mzumbe imeibuka mshindi wa mashindano ya mpira wa kikapu katika mashindano ya mpira huo yaliyofanyika St. Jordan University college iliyopo nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Mashindano hayo yamejumuisha Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Mzumbe na St. Jordan yalikuwa mashindano makali kiasi cha kutoana jasho lakini hata hivyo kwa kuwa mshindi siku zote lazima apatikane, Mzumbe waliibuka kidedea mbele ya SUA na kubeba kombe hilo.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa hisani ya Benk ya CRDB yamejumuisha pia mchezo wa mpira wa Miguu na Pete ambapo Mzumbe waliibuka washindi wa pili na kupata kikombe cha mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa miguu pamoja na medali za shaba baada ya kushindwa kwa magoli mawlili kwa Nunge (Mzumbe 0, St. Jordan 2) katika mchezo wa fainali, pia katika mpira wa pete Mzumbe imejinyakulia medali za shaba kwa kuwa mshindi wa pili nyua ya St. Jordan netball Team ambayo imeshika nafasi ya kwanza kwa pointi 45 ambapo Mzumbe Netball Team imepata point 40 na kufuatiwa na SUA netball Team iliyopata jumla pointi 20.
Katika mashindano hayo Mzumbe imefanikiwa kumpata mchezaji bora wa Kikapu Mzee wa kudanki (Emmanuel) na kuzawadiwa medani ya dhahabu. Aidha kulikuwa na mkali wa kucheza na maiki, mtangazaji bora mwenye kipaji cha pekee kutoka Mzumbe ambaye ameongoza matangazo ya mpira wa miguu kwa kushirikiana na vyombo vya habari, Mbaraka Tombo ambaye ameibuka na medani ya Shaba kwa kuwa mtangazaji bora wa vyuo vyote vitatu.
PICHA KATIKA MATUKIO
![]() |
Marefarii wasaidizi mpira wa pete wakiwa kazini |
![]() |
Timu ya mpira wa pete St. Jordan University college wakiwa kwenye pozi |
![]() |
Timu ya mpira wa pete ya SUA iliyoshiriki mashindano. |
![]() |
Timu ya Mpira wa pete ya Mzumbe ikiwa kwenye picha na Naibu Waziri wa Michezo Mzumbe, Mh. Robert Tende (Kushoto) na Kulia ni Ndugu Maganga, Refarii wa mchezo huo wa Pete kutoka St. Jordan |
![]() |
Timu ya mpira wa Miguu ya Mzumbe ikiwa kwenye pozi pamoja na Waziri wa Michezo (kulia) Mh. Dennis Kato |
![]() |
Timu ya mpira wa volleyball ikiwa kazini (Kushoto ni Timu ya Mzumbe) |
No comments:
Post a Comment