Mh. Amon Chakushemeire Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (MUSO) akisoma hotuba yake kwenye Baraza la Wanachuo wa Chuo Kikuu Mzumbe, hotuba hiyo imewavutia wanachuo kwani imegusa matarajio yao kwa kiasi kikubwa na walionekana kufuatilia kwa makini na pia ilipongezwa na wanachuo hao ambao walipata nafasi ya kutoa maoni na kuuliza maswali. Kati ya mambo yaliyokonga mioyo ya wanachuo ni pamoja na suala la mabadiliko ya sheria za mitihani, Mikopo ya wanachuo kutoka bodi ya Mikopo hasa kwa kuwa walikuwa na shauku ya kujua hatima ya wanafunzi waliositishiwa mikopo yao kwa kupata "Supplementary", ambapo aliwahakikishia kuwa lilikuwa limeshashughulikiwa na wangeendelea kupata mikopo yao baada ya taratibu zote kukamilika, Aidha amewataka wanafunzi kuelewa mipaka ya Viongozi wao katika kufuatilia baadhi ya mambo na kuwaondoa wasiwasi wanachuo kwa kuwaomba wapuuze baadhi ya fikira potofu kutoka kwa watu wanaotaka umarufu wa kisiasa kwa madai kuwa Serikali haiwajali na kuwa haifuatilii matatizo yao na baadala yake kujenga utamaduni wa kufuatilia mambo muhimu kwa kupata taarifa kutoka sehemu husika (Viongozi wao) na si maneno yanayosemwa na wanafunzi wenzao. Akiongea kwa masikitiko makubwa alitoa mfano wa baadhi ya Habari ambayo ilikuwa ni ya uzushi na ambayo iliusikitisha Uongozi wa Chuo ya kuwa Chuo kilikuwa kikiweka pesa kwenye "fixed Account" zinazotoka Bodi ya Mikopo na kuwacheleweshea wanafunzi kwa makusudi, jambo ambalo halikuwa sahihi. |
No comments:
Post a Comment