Kikao cha Bunge la Serikali ya Wanafunzi (MUSO) kimefanyika na kumalizika kwa kuchagua tume huru ya Uchaguzi ambayo inaundwa na wajumbe kumi ambao walimchagua Mwenyekiti wa Kamati hiyo, makamu mwenyekiti na Katibu wa Kamati hiyo.
Bunge hilo ambalo lilikuwa ni la Mwisho limeahilishwa kwa kuvunjwa na Mh. Rais wa Serilkali ya Wanachuo (MUSO).
Bunge limeanza kwa utangulizi wa hotuba ya Mh. Frenk Mbialu (Spika wa Bunge la Serikali ya Wanachuo - MUSO), ameanza kwa kuwashukulu wabunge kwa kuonesha Ushirikiano kwa kipindi chote chake cha Uongozi kilichomalizika baada ya Rais kulihotubia na kulivunja Bunge hilo. Katika hotuba hiyo ya utangulizi aliwasihi sana Wabunge kupitisha Sheria ya Matumizi ya fedha ili kuleta dhana ya uwajibikaji kwa serikali itakayokuwa madarakani kwa Mwaka wa masomo 2013 na ndpo alipomkaribisha Waziri Mkuu kufungua kikao hicho rasmi.
Waziri Mkuu ameanza kwa kutoa taarifa ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO ) ambao Rais wa MUSO aliibuka Mshindi na kuwa Mwenyekiti wa TAHLISO, hivyo amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TAHLISO. Pia alichukua nafasi hiyo kuwashukulu Wabunge kwa Ushirikiano waliouonesha kwa kipindi chote Serikali ilipokuwa madarakani.
Miswada mbalimbali imejadiliwa katika Bunge hilo, miswaada iliyotawala katika Bunge hilo ilikuwa ni pamoja na ule wa Sheria ya matumizi ya fedha, mapendekezo ya mchango wa TShs 5000/= itakayokuwa inakatwa kwenye pesa ya "Caution money" ambao unalenga kuchangia ujenzi wa mabweni, kusaidia wanafunzi wenye matatizo na gharama za masomo kwa Wanachuo wanaosoma nje ya nchi katika prrogramu ya kubadilishana (Exchange programs), michango ilipendekezwa na jumuiya ya wanachuo waliohitimu Mzumbe (Mzumbe University Convocation). Mswaada mwingine ni pamoja na ule wa Mchango wa Bima ya kifo (Funeral Assurance) TShs. 2500/= kuchangiwa na wanachuo, pendekezo lililoletwa kwa Serikali ya wanachuo na Kampuni ya AFRICAN LIFE ASSURANCE ambayo makao yake makuu ni Afrika ya Kusini ambapo mwanachama anayefariki familia yake hufaidika kwa kupewa TShs. 800,000/=.
Miswaada yote imejadiliwa na Mswaada wa Sheria ya Matumizi ya fedha umepitishwa kwa mapendekezo kuwa sheria hiyo ifanyiwe marekebisho baadhi ya vipengele vyenye mapungufu. Mswaada wa Michango ya Funeral Assurance na ule wa michango uliopendekezwa na jumuiya ya Wanachuo wa Mzumbe waliohitimu miaka ya nyuma haikuweza kupitishwa. Wabunge walipendekeza kuwa Miswaada hiyo ijadiliwe kwenye Baraza la wanachuo na kuletwa Bungeni katika Bunge linalofuatia ili ijadiliwe.
Wabunge wamefanikiwa kuchagua Kamati ya Uchaguzi itakayoratibu Uchaguzi wa Viongozi wa MUSO (FRs, SRs, Senators na Rais), Tume hiyo inayoundwa na ajumbe kumi (10) ilifanikiwa kumpata Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi pamoja na Katibu wa kamati hiyo. Aliyefanikiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti ni Mh. Mashibanda, Mwenyekiti Msaidizi ni Ester Charles na nafasi ya katibu imechukuliwa na Paul Samwel.
Mh. Rais wa Serikali ya Wanachuo, Amon Chakushemeire ameahilisha na kuvunja Bunge kwa kuainisha mafanikio ambayo Serikali imeyatekeleza kwa kipindi chake cha Uongozi ikiwa ni pamoja na Matokeo ya wanachuo kutolewa kwenye ARIS, kuiunganisha MUSO na jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (EAUSC) na TAHLISO, kuunganisha DSTV ambapo wanachuo huangalia mpira bure, Mifumo ya sauti (Audio systems)vyumba vya mihadhara, kuimalishwa kwa mfumo wa Intanet, Makongamano ya kitaaluma, kupunguza gharama ya mawasiliano kwa kushilikiana na mitandao mbalimbali mfano Airtel (mfumo wa Boom) ambao umepunguza gharama za mawasiliano kwa kiwango kikubwa, kuwagharimikia gharama za chakula (mill accomodation) wanafunzi wanne kutekeleza sera ya Serikali ya kuwapa nafasi wanawake ambapo Serikali yake iliindwa na asilimia 55% ya Wanawake, NMB ATM na kubwa zaidi kufanikiwa kupata Sheria mpya za mitihani.
Mwisho Rais amewaponongeza wajumbe waliochaguliwa katika tume ya Uchaguzi na kuwashukulu wabunge kwa kutoa Ushirikiano mzuri kwa kipindi chake cha Uongozi ambacho kilikuwa kinaelekea kumalizika ndani ya mwezi mmoja baada ya Rais kuapishwa. amemaliza kwa kutoa angalizo na ushauri kwa baadhi ya wabunge kujitambua kuwa wao ni sehemu ya Serikali na hivyo kutokuonesha hali ya Usariti katika Serikali ijayo.
Bunge limevunjwa rasmi na Mh. Rais wa MUSO na kabla ya kuvunja bunge hilo alitanguliwa na hotuba ya Mh. Frenk Mbialu (Spika wa Bunge la Serikali ya Wanafchuo Mzumbe (MUSO). Katika hotuba yake ya
mwisho kwa Bunge amempongeza Rais kwa kuiongoza Serikali kwa mafanikio makubwa
hasa kwa kufanikiwa kutunga sheria ya Matumizi ya fedha iliyopitishwa kwa
kishindo, kufanikisha kupatikana kwa sheria mpya za mitihani kutekeleza baadhi ya ahadi alizoahidi katika ilani yake.
PICCHA KATIKA MATUKIO
![]() |
Mh. Chakushemeire, Rais wa Serikali ya wanafunzi MUSO akisoma hotuba yake Bungeni, hotuba iliyofuatiwa na kuvunjwa kwa Bunge la Serikali ya Wanafunzi la mwaka 2012. |
![]() |
Mh. Frenk Mbialu, Spika wa Bunge la Serikali ya wanafunzi MUSO akifungua kikao cha Bunge. |
![]() |
Mh. Kamihanda (Mbunge) akichangia hoja ya Mswaada wa Sheria ya matumizi ya Fedha. |
![]() |
Wabunge wakila kiapo cha utii cha kuitumikia Serikali ya Wanafunzi (MUSO). |
![]() |
Waheshimiwa Mawaziri wa Serkali ya Wanafunzi (MUSO) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais . |
![]() |
Mh. Justus, Waziri wa fedha akiwasilisha Bungeni Mswaada wa sheria ya matumizi ya fedha. |
![]() |
Mh. Kanduru, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO) akifungua kikao cha Bunge. |
![]() |
Wabunge wapya wakila kiapo cha kuitumikia Serikali ya Wanafunzi (MUSO). |
![]() |
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi MUSO, Ndugu Mwashibanda Lukas Shibanda |
![]() |
Makamu Mwenyekiti Uchaguzi MUSO, Ndugu Ester Charles |
![]() |
Katibu wa Tume ya Uchaguzi MUSO, Ndugu Paul Samwel |
No comments:
Post a Comment