Mh. Rais wa Serikali ya wanafunzi Mzumbe (MUSO) akiwahutubia wanafunzi kwenye mafunzo ya awali (Orientation) inayowaandaa wanafunzi kuyajua mazingira, mbinu mbalimbali za kukabiliana na masomo ya Chuo Kikuu na kuwafahamu Viongozi mbalimbali wa Chuo. Rais amewakaribisha na kuwapongeza kwa kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe pia amewahakikishia kuwa serikali yake iko imara na iko tayari kuwawakilisha vema matatizo na changamoto zao kwa uongozi wa Chuo kwani ndiyo Shughuli ya serikali ya Wanafunzi. Amewataka wanafunzi wote kufikisha matatizo yao mahali husika. Zaid amewakumbusha kuwa matatizo ya wanafunzi wa Mzumbe yanatatuliwa kwa kukaa meza moja ya mazungumzo na kufikia muafaka hivyo amewataka kutumia fursa ya mazungumzo kufikia muafaka wa matatizo yao. (Katika picha; Kushoto ni Makamu wa Rais Bi. Delvina Mushi na Kulia ni Katibu Mkuu wa Serikali ya MUSO Bi. Shemsa). |
No comments:
Post a Comment