Monday, October 22, 2012

Ndugu Amani (Mtaalamu wa ICT Mzumbe akifafanua juu ya matumizi  ya  Google  Apps  kwa  wanafunzi  wa  mwaka  wa  masomo 2012/2013 katika moja ya mafunzo yaliyotolewa katika mafunzo ya awali na kitengo cha Teknohama Mzumbe.

Mwalimu Ghasia (Mkurugenzi Mwandamizi wa Idara ya habari na Mawasiliano) akifundisha matumizi na umuhimu wa E-learning wanzafunzi wa  mwaka wa  masomo  2012/2013 katika mafunzo ya awali. 

Ndugu Albert (Naibu Waziri wa Habari na Mawasiliano akifafanua kuhusu  Blog  mpya  ya  MUSO  (Mzumbe  University Student  Organization) ambayo imelenga kutumika katika kupashana habari kati ya wanafunzi na Serikali yao juu ya matukio mbalimbali na kubadilishana mawazo pia kutoa maoni yao mbalimbali.

Bi. Domitila (Google Ambassador) akiwafundisha wanafunzi  matumizi  na  umuhimu wa  Google  Apps for  Education  Services.

Dr. Msabila (Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano)  Mzumbe  akitoa  mafunzo  ya  awali  kwa  wanafunzi wa  mwaka wa masomo 2012/2013 juu ya Teknohama na faida zake ambapo amefundisha matumizi ya ARIS na E-LEARNING. Wanafunzi walionekana kufurahia na kufuatilia kwa makini sana somo hilo kiasi cha kuomba liendelee kufundishwa mara kwa mara Chuoni. 

Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa  mafunzo  ya  awali  ya  Habari na Mawasiliano  

Sunday, October 21, 2012

Mh. Rais wa Serikali ya wanafunzi Mzumbe (MUSO) akiwahutubia wanafunzi  kwenye mafunzo ya awali (Orientation) inayowaandaa  wanafunzi kuyajua mazingira, mbinu mbalimbali za kukabiliana na masomo ya Chuo Kikuu na kuwafahamu Viongozi mbalimbali wa Chuo. Rais amewakaribisha na kuwapongeza kwa kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe pia amewahakikishia kuwa serikali yake iko imara na iko tayari kuwawakilisha vema matatizo na changamoto zao kwa uongozi wa Chuo kwani ndiyo Shughuli ya serikali ya Wanafunzi. Amewataka wanafunzi wote kufikisha matatizo yao mahali husika. Zaid amewakumbusha kuwa matatizo ya wanafunzi wa Mzumbe yanatatuliwa kwa kukaa meza moja ya mazungumzo na kufikia muafaka hivyo amewataka kutumia fursa ya mazungumzo kufikia muafaka wa matatizo yao. (Katika picha; Kushoto ni Makamu wa Rais Bi. Delvina Mushi na Kulia ni Katibu Mkuu wa Serikali ya MUSO Bi. Shemsa).

Mawaziri na Makatibu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba  ya  Mh. Rais  wa  Serikali  ya  wanafunzi  Mzumbe (MUSO).

Friday, October 19, 2012

Profesa Daniel Mkude (Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu  Mzumbe)  akiwaeleza  wanafunzi  wa  mwaka wa  masomo  2012/2013 shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bodi hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia raslimali za Chuo, kuhakikisha wanafunzi wanajifunza katika mazingira mazuri, Kutunga Sheria ndogondogo za Chuo (by Laws), kupitisha mapendekezo mbalimbali yanayotolewa na Uongozi wa Chuo katika vikao vyake vinne vinavyofanyika kila mwaka, mfano kama kuna uhitaji wa kuongeza vitivo (faculties/Schools) pia amewasisitizia wanafunzi kuzingatia masomo ili kufikia malengo yao binafsi na yale ya Chuo. (Kutoka kulia ni Rais wa Serikali ya MUSO, Msaidizi wa Mshauri Mkuu wa Wanafunzi (Assisstant Dean Of Students), DVC Finace and Administration, Mweyekiti wa Bodi ya Chuo na DVC Accademic).

Porfesa Itika (Kaimu Makamu mkuu wa Chuo - DVC Accademic) akiwahutubia wanafunzi wa mwaka wa masomo  2012/2013  

Profesa Kamuzora (Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo - DVC Finance and  Administration)  akihutubia wanafunzi katika ukumbi wa NAH kwenye mafunzo ya awali kwa mwaka wa masomo 2012/2013

Wanafunzi wa mwaka wa masomo 2012/2013 wakifuatilia hotuba za Makaimu Wakuu wa Chuo  Kikuu  Mzumbe  kwenye  kipindi cha mafunzo ya awali (Orientation),  Makaimu wote wamewakaribisha wanafunzi na kuwapongeza kwa kuchaguliwa kujiunga na chuo Kikuu cha Mzumbe, aidha wamekumbushwa kutojihusisha na masuala ya siasa ya vyama na udini ndani ya Chuo.

Zoezi la Usajiri likiendelea katika ukumbi wa mihadhara (LT 1)  Kulia ni  Maofisa  wa  Idara  ya  fedha  Mzumbe  na  Kushoto Ni wanafunzi wapya wakiendelea na Usajiri. Zoezi hilo limepongezwa na Uongozi wa Chuo pia na wanafunzi kuwa limekuwa la kipekee na mafanikio ya hali ya juu. Aidha Serikali ya wanafunzi( MUSO), Idara ya Fedha na Vitivo wamepongezwa na Kaimu Mkuu wa Chuo kwa kufanikisha zoezi la Usajiri kwa ufanisi.

Msaidizi wa Mshauri Mkuu wa wanafunzi (kulia) na Naibu Waziri  wa  Elimu  (kushoto)  pamoja  na  wanafunzi  wakifuatilia kwa makini  hotuba za Makaimu Wakuu wa Chuo kikuu Mzumbe.

 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

IDADI YA WASOMAJI

RedEnvelope
. .

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...