Na Albert Nzilolela
Rais mteule, Mh. Lukiko
Lukiko wa Serikali ya wanafunzi Mzumbe (MUSO) ameapishwa katika ukumbi wa NAH na
kufuatiwa na hafla ya kumpongeza iliyofanyika katika hotel ya Lumumba Complex
Mzumbe. Kabla ya kuapishwa, alitanguliwa na hotuba ya Rais anayemaliza kipindi
chake cha uongozi na Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi. Mgeni Rasmi katika hafla
hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyewakilishwa na Afisa Utumishi wa Mkoa
Ndugu Elias Andrew.
Rais anayemaliza muda
wake Mh. Amon Chakushemeire amewashukulu sana wanachuo kwa kumuamini na
kumchagua kuiongoza Serikali ya wanachuo (MUSO). Katika hotuba yake ameushukulu
uongozi wa Chuo pamoja na Baraza la mawaziri na Bunge la wanachuo kwa kumpa
ushirikiano wa hali juu kwani anaamini kuwa ushirikiano huo ndiyo umepelekea yeye
kumaliza muda wake kwa heshima kubwa na mafanikio makubwa. Pia alionesha
kusikitishwa na dhana ya wanachuo kudhani kuwa wana ufahamu wa kila jambo kwa
kutojali kusoma hata matangazo yanayowahusu suala linalopelekea kutokuhudhuria
semina na midahalo mbalimbali inayofanyika chuoni. Lakini pia amekiri kuwa ni
kazi ngumu sana kuwaongoza wasomi.
Mwenyekiti wa tume
amezungumzia changamoto mbalimbali zinazoikumba tume ya uchaguzi ikiwa ni
pamoja na bajeti finyu kwa ajili ya kuendeshea shughuli za uchaguzi, upatikanaji
wa taarifa za wanafunzi kwa muda, wanafunzi
kutokuwa na hulka ya kusoma matangazo suala ambalo lilipelekea wagombea
wengi kurejesha fomu za kuteuliwa kuwa wagombea kwa kuchelewa, upatikanaji wa
mwenyekiti wa tume kwa kigezo cha kuwa mtu mwenye uelewa au taaluma katika masuala
ya sheria kuwa kinawanyima haki wanachuo wengine kugombea nafasi hiyo.
Baada ya hotuba ya
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Rais mteule na makamu wake Mh. Teddy Ladislaus wameapishwa
na kufuatiwa na hotuba ya Rais huyo, Mh. Lukiko Lukiko. Katika hotuba yake
amewashukulu wanachuo kwa kumpa nafasi hiyo kubwa ya kuiongoza serikali ya
MUSO. Aidha, Rais Lukiko amesema kuwa anaamini kuwa njia sahihi ya kufanikisha
jambo lolote ni kwa njia ya majadiliano na ushirikiano.
Aidha Rais Lukiko amewahakikishia wanachuo waliofika katika hafla hiyo ya kuapishwa kwake kuwa
angejitahidi kuweka mazingira bora ya kuwafanya wanachuo wapate mafanikio
mazuri kitaaluma. Amegusia mambo mbalimbali ya kijamii kama vile unyanyapaaji
wa waathirika wa UKIMWI, Rushwa, Chuki zinazotokana tofauti za kisiasa pamoja
na mifumko ya bei za vitu. Ameahidi kuandaa midahalo mbalimbali ya majadiliano
ili kutoa elimu juu ya changamoto hizo ambazo ni vikwazo vya maendeleo pia
ametoa wito kwa wasomi kutumia elimu yao kusaidia jamii zinazowazunguka hasa
watu wa vijijini.
Hotuba ya Rais Lukiko
imefuatiwa na hotuba ya Profesa Kamuzora (Kaimu Makamu mkuu wa Chuo) ameipongeza
serikali iliyomaliza muda wake kwa umahili mkubwa na ufanisi katika utendaji
kazi wake na kumaliza muda wake pasipokuwa na matatizo yoyote na kukili kuwa
hakuamini kuwa muda wa uongozi ulikuwa umeisha kwani aliona kuwa ni muda mfupi
sana kwa kusema kuwa ameona kama siku zilikuwa zimekimbia sana kwa upande
mwingine amempongeza Rais aliyekuwa anamalizia muda wake Mh. Amoni
Chakushemeire kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TAHLISO na kusema kuwa hiyo
inadhihirisha kuwa ni Kiongozi bora na mtu anayekubalika si ndani ya chuo bali
hata nje ya mipaka ya chuo pia amempongeza Rais mpya Mh. Lukiko Lukiko kwa
kuaminiwa na kuchaguliwa na wanachuo na kusema kuwa amechaguliwa kuwaongoza
wanachuo hivyo hana budi kuwatumikia kwa bidii. Amewashauri wanafunzi kujenga
tabia ya kutumia “website” ya chuo na “blog” ya MUSO kupata taarifa mbalimbali
zinazohusiana na chuo kwani suala la matumizi ya mbao kwa ajili ya matangazo
litasitishwa mara moja hivi karibuni.
Baada ya hafla hiyo ya
kuapishwa lilifuatia tukio ya sherehe ya kumpongeza iliyofanyikia katika hoteli
ya Lumumba Complex iliyoko Mzumbe. Katika sherehe hiyo wazazi walipata fursa ya
kumpongeza Rais Lukiko. Baba mzazi, Ndugu Ilvin Mgeta amempongeza mwanae na
keahidi kuwa atampa ushirikiano katika kipindi chake cha Uongozi, pamoja na
pongezi hizo amemtahadharisha Rais Lukiko kuwa kazi aliyopewa ni kubwa na ina
majukumu makubwa hivyo amemtaka kutumia muda wake vizuri ili kuhakikisha
haporomoki kimasomo.
MATUKIO KATIKA PICHA
![]() |
Mh. LUKIKO LUKIKO (RAIS MTEULE WA SERIKALI YA WANAFUNZI) AKIAPISHWA |
![]() |
Mh. TEDDY LADISLAUS (Makamu wa Rais wa Serikali ya wanachuo MUSO) AKIAPISHWA |
![]() |
Mh. Lukiko Lukio Rais Mteule (kulia) akiwa na Mh. Amon Chakushemeire (kushoto) Rais anayemaliza muhula wake |
![]() |
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Ndugu Mwashibanda Shibanda akitoa tathmini ya Uchaguzi wa mwaka 2013 |
![]() |
Mama mzazi wa Rais Lukiko, Mrs. Yusta Mgeta akimpongeza mwanae kwa kuchaguliwa |
![]() |
Baba mzazi wa Rais Lukiko, Ndugu Ilvin Mgeta akimpongeza mwanae katika sherehe ya kumpongeza Rais iliyofanyika Lumumba complex. |
![]() |
Baadhi ya Viongozi wa MUSO (mbele) na wanachuo wakishuhudia Rais wa Serikali ya MUSO pindi akiapishwa |
![]() |
Viongozi wa MUSO wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali ya kuapishwa kwa Rais Lukiko. |